Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linex amemtaka mwanamuziki mwenzake Baba Levo kuacha mara moja kumuongelea maisha yake mara kwa mara kwenye vyombo vya habari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Linex amemchana Baba Levo kuwa aache kuongelea maisha yake au kuzungumzia maisha yake ya nyuma.
Linex ameandika Baba Levo achaga kuongea ongea Mambo zangu Au past zangu kwenye Radio plzzz Live me alone Bro Na Kama Kuna sehem nilikukosea Nisamehe namaanisha Kuna Vitu kibao Vya Kuongea au Kuzungumzia usinifanye Content plz Nina Maisha Nje Ya Kujulikani’.
Linex na Baba Levo ni marafiki wa miaka mingi na Baba Levo ameshawahi kukiri mara nyingi kuwa Linex ni kati ya watu ambao walimsaidia miaka ya nyuma alipokanyaga ardhi ya Dar es Salaam kupambania kipaji chake cha muziki.
Baba Levo amekuwa akifunguka matukio na tabia za Linex ambazo walikuwa wanazipitia miaka ya nyuma. Si hivyo tu Baba Levo amekuwa akilitaja jina la Linex kwenye mifano mbalimbali afanyapo mahojiano na vyombo vya habari jambo ambalo linamfanya Linex kukwazika.