Mwanamuziki wa Bongo fleva, Sunday Sangu maarufu kama Linex ‘Sunday Mjeda’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mzazi mwenzake amempora Mtoto Wake.

Linex ameeleza kisa cha mwanamke ambaye alikuwa Mpenzi Wake na kuzaa naye kumgeuka na kumchukua Mtoto wao ambaye hajamuona kwa miaka kadhaa sasa.

Linex amesema kuwa hajamuona mtoto wake huyo wa kiume takribani miaka minne iliyopita tangu aliponyang’anywa nyumbani kwa mama yake.

Inadaiwa sakata hilo lilitokea Baada ya Linex na mzazi mwenzake kuvurugana ndipo mwanamke huyo alibeba kilicho chake na kuondoka na Mtoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *