Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amekanusha tetesi za kuachana na mpenzi wake ambaye ni mzazi mwenzake anayefahamika kwa jina la Shaban Mchomvu.
Linah amesema kuwa hajaachana na mume wake huyo hivyo tetesi za kuachana hazina ukweli wowote bali watu wanasambaza habari hizo kwa kuwa hawana mapenzi ya dhati na yeye.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa anasikia yote yanayozungumzwa lakini anakaa kimya kwakuwa yeye na baba wa mtoto wake wana familia hivyo hawezi kulichukulia kwa undani mana siyo kweli.
Linah amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote watu wanatengeneza tu na ndio maana yeye amenyamaza kimya.
Siku chache zilizopita zilienea taarifa kuwa Linah ameachana na mpenzi wake huyo ambaye amezaa nae mtoto mmoja wa kike.