Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah amefunguka suala la kubadili dini iwapo atatakiwa kufunga ndoa na baba mtoto wake maarufu kwa jina la mchomvu ambaye ni muislamu.

Wawili hao ambao wako pamoja na wanaishi pamoja huku wakiwa na imani tofauti za dini, mpaka sasa hawajafunga ndoa kuhalalisha mahusiano yao.

Watu wengi wamekuwa wakihisi huenda linasababishwa na utofauti wa dini, na kutaka kujua juu ya suala hilo la dini.

Linah amesema kuwa watu wamezoea kubadili dini kwa ajili ya mapenzi, lakini inatakiwa kubadili dini kwa uamuzi wako mwenyewe na sio sababu ya kitu fulani.

Suala hilo bado linaleta hali ya sintofahamu kama iwapo Linah atabadili dini klumfuata baba mtoto wake ambaye ni Muislam, huku yeye Linah akiwa ni Mkristu aliyetokea kwenye familia ya kichungaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *