Mwanamuziki wa Marekani, Lil Wayne uhenda akafungwa miaka 10 gerezani akikutwa na hatia baada ya kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria, kukutwa na madawa ya kulevya aina cocein na bangi.
Shtaka hilo ni la tukio lililotokea mwezi Desemba 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Miami Opa, Marekani, baada ya polisi kufanya upekuzi ndani ya ndege ya msanii huyo. Kesi ya rapa huyo ilisomwa jana Jumanne Novemba 17 huko Miami nchini Marekani.
Bosi huyo wa lebo ya Young Money, amekana mashtaka hayo na kesi yake itasomwa tena mwakani, 2021.
Hatua hii imekuja siku chache tangu rapa huyo alipotangaza kumuunga mkono Rais Donald Trump kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi huu.
Kitendo hicho kilimfanya mpenzi wake, Denise Bidot, kutangaza hadharani kuchukizwa na kitendo hicho na kuamua kuachana naye japokuwa baada ya Joe Biden kushinda alisema amemsamehe na kurudisha mahaba tena.