Klabu za ligi ya China zitaruhusiwa kuchezesha wachezaji watatu wa kigeni kwa kila mechi kwenye msimu mpya utakaoanza mwezi machi mwaka huu.
Sheria hiyo imekuja ili kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa kwenye ligi hiyo kutoka barani Ulaya ili kukuza wachezaji wa ndani ya nchi hiyo.
Hapo awali sheria ilikuwa “4+1” mana yake wachezaji wanne wa kigeni kutoka taifa lolote na mchezaji mmoja kutoka ndani ya bara la Asia kwenye kikosi.
Viungo wa Chelsea na John Mikel Obi wamejiunga na ligi ya China pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Bocca Junior, Carlos Tevez na kajiunga na ligi hiyo katika klabu ya Shanghai Shenhua.
Klabu ya Shanghai Shenhua ni miongoni mwa klabu zitakazoathrika na sheria hiyo kutoka na kuwa na wachezaji sita wa kigeni ndani ya kikosi chao kuanzia, Carlos Tevez, Demba Ba na Obafemi Martins.