Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amemtaka Rais , Dkt. John Pombe Magufuli kuiga mfano wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo.
Lema alimsifu Rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda
Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinzani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.
Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.
Lema amesema kuwa kuruhusiwa kwa maandamano na mikutano ya kisiasa kuna faida ya pande zote mbili yaani upande wa chama tawala na upnde wa upinzani hivyo matokeo yake hunufaisha pande zote.