Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema amemjibu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu kauli aliyotoa jana kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu endapo familia yake itaomba kwa serikali.
Lema amesema kuwa familia ya Lissu hajashindwa kumgharamia matibabu kwani wapo tayari kwa kila kitu juu ya maibabu ya Lissu.
Lema amesema kuwa anaamini familia ya Tundu Lissu ni Watanzania wote ambao wanapenda haki na Demokrasia ndani ya nchi, na wote ambao wanaumizwa na jambo hilo bila kujali itikadi zao hivyo watachanga shilingi moja moja kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu na hata ikibidi mali zao watauza ili kuweza kumuwezesha Tundu Lissu kupata matibabu.
Jana Septemba 21, 2017 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa Tanga alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia yeye imemuhakikishia Mhe. Tundu Lissu na familia kuwa ipo tayari kugharamia matibabu yake zaidi pindi tu watakapopata maombi kutoka kwao.