Klabu ya Leicester City imemtimua Kocha wake, Claudio Ranieri baada ya mwenendo mbaya kwenye ligi kuu nchini Uingereza.
Leicester ipo nafasi ya 17 alama moja tu kufika kwenye mstari wa kushuka daraja kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi hiyo.
Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Sevilla kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.