Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya shirika la fedha duniani IMF, Abebe Selassie amesema kwamba kushuka kwa bei ya mafuta  katika miaka miwili iliyopita imesababisha nchi nane za Afrika kushuka kwa uchumi.

Naibu Mkurugenzi huyo amezitaja nchi zilizoathirika zaidi kuwa ni pamoja na Angola, Equatorial Guinea na Nigeria ambazo zimeshuhudia kushuka kwa bei ya mafuta kutoka dola 125 kwa pipa hadi dola 50.

Athari ni pamoja na kupungua kwa kasi ya mapato ya kuuza bidhaa nje na nakisi ya fedha.

Hata hivyo kushuka kwa bei ya mafuta kumekuwa na faida kwa nchi ambazo zinatarajia kuzalisha mafuta kama Tanzania na Msumbiji kwa kuwa nchi hizo hazijaanza kuzalisha mafuta hivyo hawataathiriki na kushuka kwa bei.

Vile vile naibu mkurugenzi huyo ametoa wito kwa watunga sera katika nchi hizo kuzingantia uchumi mseto kama uzalishaji wa nishati, ukuzaji wa sekta ya kilimo ili kuepuka na kutegemea mapato ya mafuta pekee.

N

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *