Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah amefunguka na kusema kuwa mahaba anayopewa na mzazi mwenzake, muigizaji Aunty Ezekiel, hakuna wa kumtoa hapo.

Kusah amesema kuwa anampenda Aunty leo, kesho na hata milele na kwamba mwendo ameumaliza kwa mama huyo wa watoto wawili.

“Kwa kweli siwezi kuwa mnafki, ukweli ni kwamba nimeshikwa na nikashikika, hakuna wa kuweza kunichomoa kwa Aunty wangu, nampenda leo, kesho na hata milele.

Kifupi kwake mwendo nimeumaliza,” anasema Kusah ambaye amejaaliwa mtoto wa kiume na Aunty waliyempa jina la Norma au Nono.

Mwanamuziki huyo kabla ya kuingia kwenye mahusiano na Aunty Ezekiel alikuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki mwenzake Ruby ambaye pia amepata nae mtoto mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *