Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah metoa maoni yake juu ya mvutano unao endelea sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii.
Kusah ameamdika “Sipo katika upande wowote na sijawahi kuwa wa Team ila kwa upeo wangu mdogo Steve Nyerere anafaa sana akipewa mda na ushirikiano haiwezekani msemaji wa Muziki wetu kutokea kwa Wanamuziki maana sisi wenyewe hatujawahi kuwa na umoja wala kupendana kiasi hicho wapembeni hawawezi kuelewa.
Ila walioko ndani wanajua namaanisha nini hao hao wakubwa tunaowategemea sijawahi hata kuona wakisaidia mtu yoyote wapembeni ambae hawaingizii kitu kwao sasa.
Pia amesema kuwa wasibaki walewale kila siku ilibidi aje mtu kutoka pembeni na hili sio baya kabisa na sidhani Kama hao wote waliomchagua hawakua timamu hebu tuheshimu mawazo Yao na tuwape mda na maana ya kuwa MSEMAJI sio kwamba haruhusiwi kushauriwa.