Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa alisita kutia saini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita kwa sababu hakuwa na uhakika kwamba angeweza kuiongoza klabu hiyo.

Wenger alikubali mkataba wa miaka miwili mwezi Mei, mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Kocha huyo amesema kuwa alikuwa na sababu za kibinafsi kutokana na uamuzi uliochelewa wa kuongeza muda wake wa miaka 21 na klabu hiyo.

Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano katika Ligi kuuu nchini Uingereza msimu uliopita, ikiwa ni mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nambari nne tangu Wenger alipojiunga na klabu hiyo mwaka 1996.

Arsenal walianza michuano ya msimu huu ya Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa nyumbani wa magoli 4-3 dhidi ya Leicester, kabla kupoteza kwa Stoke kwa goli 1-0 na Liverpool 4-0.

Wenger pia aliulizwa, kuhusiana na aliyoyafanya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Monaco, 21, Thomas Lemar.

Ada iliyoripotiwa na kukubaliwa ilikuwa £90m, lakini Wenger alisema kwamba mchezaji huyo ”aliamua kusalia Monaco”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *