Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofi kiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.

Majaliwa aliyasema juzi baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli jijini Kigali, Rwanda, ambapo alisema Tanzania imejiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali, Majaliwa alisema Tanzania itahakikisha mkataba huo unatekelezwa bila kuathiri huduma zinazozalishwa ndani.

Amesema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu, ambayo imesainiwa inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.

Mikataba iliyosainiwa na mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara la Afrika kuwa eneo huru kibiashara, itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo, ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanya kazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.

 

Azimio la tatu ni Azimio la Kigali, ambalo limejumuisha mawazo ya uanzishwaji wa mchakato huo. “Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa kutia maanani suala hili hadi kufikia hatua hii ya kusaini mkataba. “Tanzania kama wadau wakuu wa mkataba huu tunakwenda kujipanga kuhakikisha unatekelezwa bila kusababisha vikwazo vyovyote.

Source: Habari Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *