Shirikisho la soka barani Ulaya, (Uefa) limetangaza nia ya kuomba nchi za Ulaya kupewa nafasi 16 kwenye mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2026.

Dhamira hiyo ya Uefa inakuja kufuatia shirikisho la soka la dunia, Fifa kupitisha azimio la kuongeza idadi ya timu kwenye mashindano hayo hadi kufikia 48.

Mbali ya kuomba idadi hiyo ya timu, Uefa pia inakusudia kuwasilisha ombi kwa Fifa la kuzitenganisha kwenye makundi timu kutoka barani humo ambazo zitafanikiwa kufuzu.

Baada ya kuidhinishwa kwa timu 48 kushiriki mashindano hayo kuanzia mwaka 2026, utaratibu uliopangwa ni kuwa na makundi 16 yatakayokuwa na timu 3 ambapo timu 32 zitafanikiwa kwenda raundi ya mtoano.

Mwaka 2014 timu 13 za Ulaya zilifanikiwa kushiriki mashindano hayo ambapo Ujerumani iliibuka bingwa.

Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin amesema kuwa maombi hayo ya Uefa ni ‘halisi’ na kila timu ya Ulaya ina nia ya kuvuka mzunguko wa kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *