Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kimesitisha uzalishaji kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.

Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Harpeet Duggal amesema wapo kwenye mazungumzo na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo.

Mwezi uliopita mkurugenzi huyo alilalamika uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo alidai yapo chini ya kiwango na bei ghali.

Pia alilalamikia shirika la maendeleo ya petroli TPDC kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alidai madai yao ya gharama kuwa juu ni ya uzushi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *