Kiongozi mkuu wa upnzani nchini Venezuela, Leopoldo Lopez ameachiwa huru kutoka gerezani baada ya kukaa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Aliondoka gerezani karibu na mji wa Caracas na kujiunga na familia yake siku ya Jumamosi baada ya kuachiwa huru.

Lopez alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2014, mashtaka ambayo ameyakanusha. Mahakama kuu inasema kuwa ameachiliwa kwa misingi ya kiafya.

Kwa upande wa rais wa nchi hiyo, Maduro alisema kuwa anaunga mkono na kuheshimu uamuzi wa mahakama lakini akataka kuwepo kwa amani.

Saa chacahe baada ya kuichiliwa Bwana Lopez aliwashauri wafuasia wake kuendelea kuandamana barabarani kumpinga Maduro.

Akielezea maisha ya mwawawe gerezani babake Lopez aliiambia radio moja ya Uhispania siku chache zilizopita kuwa aliadhibiwa kwa kufungiwa katika chumba kisicho na mwangaza na maji kwa muda wa siku tatu.

Alisema kuwa mwamawe sasa alikuwa amefungiwa kifaa cha eletroniki ili mamlaka ziwezi kufuatilia mienendo yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *