Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Urusi, Alexei Navanly amekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga ufisadi aliyoandaa kwenye mji mkuu Moscow.

Waandamanaji walijaribu kulizuia gari kumpekeka mwanasiasa huyo baada ya kukamawa nchini humo.

Navalny ni maarufu kwa kampeni zake za kupinga ufisadi ambazo huwalenga maafisa wa vieo vya juu walio karibu na serikali ya Urusi.,

Anazuiwa kuwania urais kumpinga rais Vladimir Putin mwaka ujao, baada ya kupatikana na hatia kati ya kesi anayoitaja kuwa ilichochewa kwa misingi ya siasa.

Waandamanaji kadha walikamatwa, pale polisi walipojaribu kuvunja maandamano katika mji wa Vladivostok, kando ya Bahari ya Pacific.

Waandamanaji huko Chelyabinsk, walitaka Waziri Mkuu, Dmitry Medvedev ajiuzulu kuhusu tuhuma za ufisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *