Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, Aboubakar Shekau amejeruhiwa kwenye shambulio la angani lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo huku makamanda wengine wakuu wa kundi hilo wameuawa.

Taarifa kutoka kwa jeshi la angani la Nigeria imesema shambulio hilo lilitekelezwa Ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.

Kwa mujibu wa jeshi makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.

Kundi la Boko Haram karibuni limekabiliwa na mzozo wa uongozi.

Kundi la Islamic State lilitangaza kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram.

Lakini muda mfupi baadaye, Shekau alisema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo na akamshtumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *