Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangalla amesema wizara hiyo ipo kwenye mchakato wa kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Jeshi jipya litakalokuwa maalumu kwa usimamizi wa wanyamapori na rasilimali za misitu nchini ili kuboresha utendaji kazi katika sekta hiyo.

Amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti na kusimamia sekta ya maliasili kutokana na kuingiliwa na majangili wanaosababisha rasilimali hiyo kuteketea.

Amefafanua kuwa jeshi litakaloundwa litakuwa chini ya Rais mwenyewe na litasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kujenga nidhamu kwa watumishi.

Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Misitu Tanzania,(TFS) Professa Dos Santos Silayo amesema kwa sasa wameimarisha utendaji wa wakala huo tofauti na ilivyokuwa awali wa kusimamia mapato  tu.

Amesema hatua ya kubadili wakala huo na kuwa mamlaka kamili ya misitu itaongeza ufanisi na utendaji kazi katika sekta hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *