Aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru leo anatarajia kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Kingunge utaagwa katika ukumbi wa Karimje jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea makaburi kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo mkongwe nchini.

Ratiba inaonysha kuwa shughuli mazishi yataanza kufanyika saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu utatolewa leo saa 10 jioni Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada na mila zitafanywa usiku mzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *