Mwanasiasa Mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema kuwa bado kuna vigogo watatu wanaotakiwa kuadhibiwa ndani ya chama hicho kwakuwa wao ndio waliosababisha mambo yote yaliyotokea.
Kingunge amewataja viongozi hao wa juu wanaopaswa kuadhibiwa kwa usaliti kuwa ni Mwenyekiti Mstaafu, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
Kingunge amesema kuwa kitendo cha kufukuzwa uanachama kwa baaadhi ya wanachama kitu hicho si kigeni kwani ni mwendelezo wa makosa yaliyojitokeza kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015.
Mwanasiasa huyo mkongwe amesema kuwa “Sophia Simba alimsaliti nani? Madabida kamsaliti nani? na katika ngazi gani? ndiyo maana nasema hili lote ni mwendelezo wa yaliyotokea 2015 kule Dodoma,”.
Kingunge amesema kuwa anashangaa sana kuona baadhi ya wanachama wanafukuzwa na wengine kupewa onyo kali kwa kile kinachoitwa usaliti, kwani wahusika wakubwa wa usaliti bado wamo ndani ya chama hicho na hawajaguswa na adhabu.