Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi madalali wa chama hicho hawatakiwi kwasasa na watafute kazi ya kufanya.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya CCM yaliyofanyika katika ukumbi wa Dodoma Convention Centre.
Kinana amesema sasa wamejipanga kuhakikisha CCM inaendelea kutawala maisha yote huku akiwataka wenyeviti wa kata, wilaya na mikoa kutokuwa na sehemu ya malalamiko na badala yake wawe sehemu ya kusimamia Serikali.
Pia Kinana amesema wamekuwa wakisimamia na kupigania haki za wananchi huku akidai kwa sasa kuna viongozi wamekuwa madalali ndani ya chama hicho.
Katibu mkuu huyo ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa vipo vyama vitatu pekee duniani ambavyo vinaoongoza kwa maandiko mazuri na yenye tija ambapo alivitaja vyama hivyo ni Chama cha Kikomunisti cha China, CCM na ANC cha Afrika Kusini.