Video Queen maarufu Bongo, Kimnana amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kuwaza kuwa siku moja atamlea mtoto wake peke yake ‘single mother’.

 

Mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mama wa binti mmoja aitwaye Sky, amesema wanaume wana mambo mengi mpaka inafikia hatua unaona bora ulee mtoto wako mwenyewe.

 

“Kusema kweli sijawahi kuwaza kuwa single mama, lakini ndiyo imetokea. Asikwambie mtu, kulea mtoto peke yako ni kazi sana, lakini Mungu mwema maisha lazima yaendelee,” alisema Kimnana.

 

Japo mwenyewe hakutaka kuzungumzia lakini inadaiwa kuwa, bibie huyo ameachana na mzazi mwenzake, mtangazaji Tony Albert maarufu kama T-Bway 360.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *