Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Killy anatarajia kuachia wimbi wake mpya baada ya kimya cha muda mrefu toka ajiunge na lebo ya Konde Gang akitokea Kings Music.
Msanii huyo ametangaza ujio wake mpya baada ya kutoka Kings Music, lebo ya msanii Alikiba na kujiunga na Konde Music Worldwide lebo ya Harmonize, mapema mwezi Septemba 2020.
Harmonize ametangaza ujio wa mwimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa instagram, huku akisema Juni 2, 2021 ni #KillyDay, akiwa na maana ndio tarehe rasmi ya Killy kuachia kazi yake tangu ajiunge na familia ya Konde Gang.
Harmonize alitudokeza kuwa album ya Killy imekamilika na tayari ana video 6 mkononi kutoka kwenye album hiyo mpya ya msanii huyo.