Rais mstaafu wa awamu ya nne ambaye ni mjumbe wa kamisheni ya kimtaifa ya elimu, Dkt. Jakaya Kikwete amefanya ziara nchini Tunisia na kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Bej Caid Essebs.
Ziara hiyo ni muendelezo wa kamisheni ya kimataifa ya elimu kuwafikia viongozi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya kazazi cha elimu (Learning Generation).
Kikwete amemkabidhi mapendezo ya ripoti hiyo kuhusu Elimu kimataifa na kuiomba Tunisia kujiunga katika mpango wa nchi za mbele kufanikisha kizazi cha elimu ifikapo mwaka 2040 katika nchi zilizopendekewa.
Kwa upande wake rais wa Tunisia Bej Caid Essebs amemuhakikishia rais mstaafu Kikwete uthabiti wa azama wa nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.
Pia rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amkutana na kufanya mazungumzo na waziri wa elimu wa Tunisia na kutembelea kituo cha uendelezaji wa teknolojia katika elimu katika elimu kilichopo Tunisia.