Kundi la Muziki wa rap, Kikosi Kazi limeamua kufanya kazi zao kwa staili tofauti itakayokuwa rahisi kueleweka na watu wa lika zote, lengo ni kuufikisha ujumbe wenye elimu ndani yake.

Kundi hilo linaloundwa na  Nikki Mbishi, P the Mc, One Incredible, Azma Mponda, Zaiid na Songa, limesema kila ngoma watakayoiachia itakuwa na ujumbe unaoishi ndani ya mioyo ya mashabiki wao.

Zaiid mmoja wa wasanii hao amesema kuwa kwamba wanafanya kazi kwa umakini na wamekuwa wana hiphop wanaopendwa zaidi na kizazi kipya.

“Mfano mzuri ngoma yetu ya Pisi Kali, ilipokelewa na kupendwa zaidi na mashabiki wetu kutokana na namna ambavyo ujumbe wetu tuliuwasilisha kwao na nimaisha halisi ya vijana wengi wa mjini ambao wanaigiza maisha;

Ameongeza kuwa “Kuna ngoma kali zinakuja ambazo zitawapa burudani mashabiki wa muziki wetu wa hiphop na kuwaleta watu wapya ambao wanapenda mziki laini kuanza kuuelewa muziki wetu ambao tunaimba kisasa,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *