Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amemjia juu waziri wa zamani wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu huku akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Dkt. Kigwangalla amesema hayo wakati akichangua Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018, Bungeni Jijini Dodoma.

Baada ya kuongea hayo Dk Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Ruswa (Takukuru kumchunguza Nyalandu.

Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Pia amemtuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *