Kiungo wa Simba, Shiza Kichuya amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga.

Kichuya amesema kwamba wapinzani wao hao ni wepesi na watawafunga leo na kuchukua alama tatu kwenye mehezo huo.

 Pia mchezaji huyo amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani bila ya hofu kwani ana uhakika wa ushindi kutokana na maandalizi yao chini ya Kocha Joseph Omog.

 Kichuya ameongeza kwa kusema kuwa katika mechi hiyo kikubwa wao kama wachezaji wamepania kupata ushindi ili waendelee kubaki kileleni katika msimamo ya ligi.

Katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita wa Februari 25, mwaka huu ambao Simba ilishinda mabao 2-1, Kichuya alifunga bao moja.

Timu hizo zinatarajia kukutana leo kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara mzunguko wa kwanza katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *