Mwanamuziki wa Taarab nchini, Khadija Kopa amesema sio jambo zuri kwa wanawake kukaa kugombea mwanaume.

Pia amewataka wawe wabunifu katika mapishi pamoja na kutumia nyonga zao ili mwanaume mwenyewe apagawe nasio kukaa kugombana.

Amesema kuwa “Unapiganaje na mke mwenzio?, yeye akirusha risasi wewe rusha atomic. Yeye akimpigia bwana chapati wewe piga mkate wa ufuta, kuku na ndizi za kupaka.

Ameongeza kwa kusema kuwa Sasa unagombanaje na mke wenzako ?,hakuna haja ya kugombana na mke mwenzio wewe fanya vitu ili mwanaume azidi mapenzi upande wako. Watu wa siku hizi hawajui bajeti ya mapenzi kazi kufofoka tu”.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema “tengeneza mambo yako nyumba inukie mambo yawe motomoto na uchangamfu kama kawaida akija mume wako afurahie, hakuna haja ya kugombana gombana kila siku wewe zidisha mavitu ili mwanaume achenguke, fahari ya mwanamke nyonga vitu vingine majaliwa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *