Mwanamuziki nyota wa taarab, Khadija Kopa amesema kuwa kwasasa mapato yake yatokanayo na muziki yamepungua kutokana na Serikali kuzuia matamasha ya muziki baada ya saa sita.
Amesema hivi sasa yeye na wenzake wapo katika mpango wa kuongea na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ili aangalie upya sheria iliyowekwa ya kufunga sehemu za starehe saa sita usiku kwa kuwa inawaumiza wasanii wa taarabu.
Amesisitiza kuwa kwa sasa biashara ya bendi za taarabu imekuwa ngumu na wanakosa mashabiki kwa kuwa muda wa kutumbuiza umekuwa mchache hivyo wanajipanga kuomba kwa mkuu wa mkoa ili siku za Ijumaa na Jumamosi ziongezewe muda hadi saa tisa usiku.
Malkia huyo wa taarab amesema sababu nyingine ni utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia majina ya wasanii wakubwa wa taarab kufanya show na kujiingizia kipato kisicho halali.
Mwanamuziki huyo wa taarab maarufu ambaye kwasasa anatamba na bendi yake inayoitwa kwa jina la Ogopa Kopa amesema kuwa ili mapato yao yaziki inatakiwa kuzidishwa kwa muda wa matamasha yao.