Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Taarab, Khadija Kopa amesema muziki huo unaonekana kama umepoteza ladha kwa sababu ya nyimbo zao kupigwa sana sehemu ya kuuza vilevi na kupotezewa katika vyombo vya habari.

Khadija amezungumza hayo akiwa kwenye uzinduzi wa video ya Saida Karoli ‘Orugambo na kusema kwamba muziki wa taarabu umeshushwa na watu wachache walioruhusu nyimbo zao kuchezwa ‘bar’ kitu kinachopelekea hata wapenzi wa muziki kususia matamasha yao yakiandaliwa.

Akizungumzia ujio wa Saida Karoli tena kwenye ‘game’ Khadija amesema sanaa ilimkosa mtu mwenye ladha ya asili kwa muda mrefu na ujio wake ni burudani kwa wasanii na wapenda muziki mzuri.

Kauli hiyo ya Saida Karoli imekuja baada ya muziki wa Taarab kupoteza dira kwenye ramani ya muziki na kusababisha kukosa show sehemu mbali mbali kwenye makumbi ya show hizo.

Khadija Kopa ambaye sasa anamiliki bendi yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la Ogopa Kopa Morden Taarab amewataka wadau wa muziki huo wakiwemo watangazaji kusaidia kurudi kwa hadhi ya muziki huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *