Beki wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy amesema kuwa rekodi za kocha mpya wa Simba, Pierre Lachantre ni nzuri sana.
Kessi ameonyesha kuwa na hofu na uongozi wa klabu hiyo kama utampatia uhuru wa kutosha kocha huyo mwenye rekodi ya kuipatia Cameroon Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2000.
Kessy amesema kuwa kama uongozi wa timu hiyo hautabadilika, kocha huyo hakuna chochote atakachokifanya klabuni hapo na badala yake ataonekana hafai kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.
Kessi amesema kuwa “Nimeisoma rekodi ya kocha huyo ni nzuri lakini kwa Simba ninayoifahamu mimi kama viongozi wake hawatabadilika basi naye anaweza kuondoka kama walivyoondoka makocha wengine waliomtangulia.
Pia amesema kuwa “Wamepita makocha wengi wazuri klabuni hapo lakini kwa sababu ya kutowapa uhuru wa kufanya kazi yao ipasavyo, walionekana hawafai, kwa hiyo hata kwa huyu kama wasipobadilika, pia ataonekana hafai,”.