Baada ya mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF)  Profesa Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama wabunge wanane, hatimaye wabunge hao wamefungua kesi mahakama kuu kupinga uamuzi huo.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakipinga kuvuliwa uanachama na mwenyekiti.

 Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo, wabunge hao wameiomba mahakama hiyo kuweka zuio la wabunge wapya kuapishwa hadi kesi ya msingi waliyofungua itakapoamuliwa.

Wabunge hao wameiomba mahakama kuzuia utekelezaji wa Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kuwavua uanachama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *