Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Mike Mushi hadi Machi 9 mwaka huu.
Kesi hiyo imeghairishwa kwa kile kilichoelezwa mahakamani hapo kuwa wakili wa upande wa Jamhuri anayeshughulika na kesi hiyo yupo likizo kwa sasa.
Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 26, 2017 na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.
Maxence Melo na Mike Mushi wanashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa domain ya .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.