Kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe na kiongozi wa maandamano Promise Mkwananzi, ya kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe imetupiliwa mbali.
Kundi la Tajamuka lilitaka kuonyesha kuwa raia Mugabe mwenye umri wa miaka 92 hayuko katika hali nzuri kuongoza kutokana na umri wake.
Mahakama ilitulipia mbali kesi hiyo ikisema kuwa bwana Mkwananzi alishindwa kumkabidhi Mugabe makaratasi ya kesi.
Sasa Mkwananzi ana siku 30 za kuchukua hatua zinazohitajika kabla ya kupeleka tena kesi hiyo mahakamani.