Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameruhusu maandamano ya upinzan kupinga matokeo ya uchaguzi nchini humo.

Kenyatta ameliagiza jeshi la polisi nchini humo kuhakikisha linayalinda maandamano ya watu hao wanaopinga ushindi wake kwani yako kikatiba.

Rais huyo anayewakilisha chama cha Jubilee amesema kuwa polisi wapo tayari kuwalinda wakati wanafanya maandamano na wale waliochukia waelewe kwamba hawahitaji kibali ccha Jubilee kufanya maandamano ya amani.

Pia amesema kuwa maandamano ya amani ni haki ya Wakenya ya kikatiba kwa wale ambao hawakuridhishwa au wamekasirishwa na mchakato husika.

Kenyatta amewataka waandamanaji kutovunja sheria kwa kufanya uharibifu wa mali au shambulio la kuwadhuru watu kwani Serikali yake haiko tayari kuona vitendo hivyo vikifanyika.

Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Agosti 8 mwaka huu dhidi ya mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *