Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameliagiza Jeshi La Polisi Kuongeza ulinzi katika Hospitali ya Agha Khan Nairobi alipolazwa Tundu Lissu.

Hii ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya usalama ili wale waovu kama watajaribu kumfuatilia tena huko Kenya basi washughulikiwe ipasavyo.

Tundu Lissu alifyatuliwa risasi 32 lakini risasi zilizompata ni tano ambapo mbili zilimpata tumboni, mbili nyingine mguuni na moja mkononi.

Kwasasa Tundu Lissu yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya matibabu zaidi katika hospitali ya Aga Khan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *