Hospitali nchini Kenya zimeanza kuwafukuza kazi madaktari wanaogoma na kuwaondoa katika wa nyumba za uma nchini humo.
Huduma kwenye hospitali za umma zimekosekana kutokana na mgomo ambao ulianza mwezi Disemba, huku madaktari na wahudumu wengine wa afya wakitaka mshahara zaidi na mazingira bora ya kufanya kazi.
Lakini hatua hiyo ya kuwafukuza kazi madaktari inakuja wakati chama cha madaktari kinasema kuwa kimetia sahihi nyaraka zinazohitajika ili kumaliza mgomo wao.
Lakini serikali imsema kuwa siku ya mwisho ya kukubali asilimia 50 ya nyongeza ya mshahara ilipita siku mbili zilizopita.
Sasa hospitali zimeanza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya madaktari ambao wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 95.