Serikali ya Kenya inatarajia kununua ndege 14 za kijeshi zenye thamani ya dola milioni 418 kutoka nchini Marekani.

Ndege hizo zitatumika katika vita dhidi ya wapiganaji wa al-Shabab wenye makao yao huko nchini Somalia ambao wamefanya mashambulizi zaidi nchini Kenya miaka ya nyuma.

Ndege hizo kwa jina Air Tractor zitaweza kukabiliana na wapiganaji hao kwa karibu ikilinganishwa na ndege za sasa za f-5 fleet.

Mauzo hayo yanachangia sera ya kigeni ya usalama ya taifa la Marekani kwa kuwa Kenya inaongoza katika eneo hilo katika vita dhidi ya wapiganaji hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *