Muigizaji wa Bongo Movie, Riyama Ally amesema kuwa anatamani yeye mumewe wazidi kupendana na waishi miaka mingi ndani ya ndoa yao.
Riyama amefunguka hayo baada ya kuwepo kwa maneno ya kugambana kwa wawili hao ambao kwasasa ni mke na mume.
Riyama amemuomba Mungu yeye na mumewe, Leo Mysterio waishi miaka mingi ili kila mmoja aje kumzika mwenzake wafikapo uzeeni.
Muigizaji huyo amesema kuwa siyo watu wote wanapenda kuombeana dua waishi miaka mingi kama mke na mume, bali huwa wanahesabu tu siku za kuachana lakini kwa upande wake yeye ni tofauti kwani anampenda sana mumewe.
Wawili hao kwasasa ni mume na mke na wanapendana sana kutokana na kutosikiliza maneno ya watu kwani walishambuliwa sana na maneno ya watu kuhusu umri wa Riyama kuwa mkubwa kuliko mumewe huyo.