Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog anahitajika zaidi na Simba kuliko hata yeye anavyohitaji Simba.

Manara  amedai kuwa Omog ni kocha pekee aliyeweza kuipa Simba vikombe viwili na kuifunga Yanga mara tatu katika mechi nne walizokutana.

Manara amesema hayo wakati akielezea mambo mbalimbali kuelekea mchezo wao na Stand United ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Kambarage Shinyanga wiki hii.

Manara amesema kuwa makocha watano wamekaa Simba wameshindwa kuwapa nafasi ya pili na wameshindwa kuwapa kikombe lakini Omog kawapa vikombe viwili na vyote kamnyang’anya Yanga.

Pia Manara amesema kuwa Simba chini ya Omog imekutana na Yanga mara nne kamfunga mara tatu, halafu watu mitaani wanasema kuwa hafai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *