Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi na kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba tayari miili ipo wenye utambuzi kwa kuchukua vinasaba ili kujua ni raia wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao kwenda kuangalia kama ni wao.
Kamanda Siro aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kwamba watu wanafikiria mauaji hayo yamefanywa na Jeshi la Polisi.
Sirro amesema kuwa Jeshi la Polisi huwa hawana kificho kama wamekutana kwenye mapambano wamewaua watu wataweka wazi kuwa wameua na siyo kwenda kuwatumbukiza baharini.
Wiki iliyopita maiti zilikutwa kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam ambapo azijulikani chanzo cha vifo vyao.