Aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesema kuwa bado ni mwanachama halali wa Chadema na CCM kwa mujibu wa Sheria kwani hakuwahi kurudisha kadi za vyama hivyo.

Kauli hiyo Dkt. Slaa ameitoa leo wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv.

Pia Slaa amesema kuwa anasikitika kwa sababu alishirika kujenga upinzani nchini na sioni chama chenye sera zilizonyooka.

Aidha kupitia mahojiano hayo Dk. Wilbard Slaa ameeleza  nia na madhumuni ya kurejea nchini na kusema kuwa amerejea kwa lengo la kushughulikia usajili wa Hospitali ya CCBRT, na kutujulisha kuwa yeye ni mwenyekiti wa hospitali hiyo.

Watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza maswali juu ya uteuzi wake na kuhoji zoezi zima la uapishwaji na kupangiwa kituo cha kazi, hivyo kwa ujio huu wangi walidhani kuwa amerejea kwa dhumuni la kuaoishwa, La-hasha.

Novemba 23, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia John Pombe Magufuli alimteua, Dk Slaa kuwa balozi ila mpaka sasa bado hajaapishwa na kupangiwa kituo cha kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *