Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bushoke Rutta amefunguka furaha yake baada ya kusikia Papii Kocha ameachiwa kwa msamaha wa Rais na kwamba ametimiza ndoto zao.
Bushoke amesema furaha aliyonayo hailezeki kwa alichokifanya Rais na haoni wa kuchukua nafasi yake, kwani alichokifanya ni kitendo cha huruma na upendo wa hali ya juu, kwa kutimiza tumaini ambalo walikuwa nalo rafiki zake hao vipenzi.
Bushoke ameendeleea kusema kwamba hivi karibuni rafiki yake huyo alimsikia akisema ana imani Rais wa sasa atawaonea huruma na kuwaacha huru, hata isingekuwa leo basi ingekuwa siku yoyote lakini waliamini hawatafikwa na umauti wakiwa jela.
Akiendelea kusimulia furaha yake Bushoke amesema aliposikia Rais anatangaza kumsamehe Babu Seya na familia yake, mwili ulimsisimka huku asiamini nachokisikia.