Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amejibu kauli ya Nandy aliposema kuwa anatamani angekuwa mke wake, na kusema kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani ingawa anaheshimu hisia zake.
Bill Nass amesema kwa sasa hawezi kujibu kwa mtazamo positive kwani kufanya hivo kutaharibu mahusiano yake ya sasa, lakini anaheshimu hisia za Nandy.
Pia amesema kuwa “Kwa coment yangu kwa sababu mtu ameelezea hisia zake kutokana labda na personality zangu, ila hanijui kiundani, siwezi kujibu in positive ingawa naheshimu hisia zake naheshimu alichokizungumza.
Billnass ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na mahusiano ambayo niko nayo siwezi kufanya move yoyote kwake, naheshimu mahusiano yangu, siwezi kucoment chochote ambacho hakitampendeza mwenzangu na hakitakuwa na mrejesho mzuri kwenye mahusiano yangu, lakini naheshimu hisia zake”.
Siku za hivi karibuni msanii Nandy alinukuliwa na moja ya chombo cha habari akisema anatamani angekuwa mke wa Bill Nass kwani anamzimia msanii huyo.