Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Marekani kutojiondoa kutoka katika mkataba wa kimataifa uliopangwa kudhibiti uwezo wa nyuklia ya Iran.

Bw. Guterres ameonya kwamba kuna hatari ya vita iwapo makubaliano hayo hayata tunzwa.

Guterres amesema makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu hayapaswi kutelekezwa isipokuwa kuwe na mbadala mwingine mzuri zaidi.

Viongozi wa Ulaya wamemtaka pia Rais Donald Trump wa Marekani kubakia katika makubaliano hayo.

Rais huyo wa Marekani aliyaita makubaliano hayo kwamba ni mkataba mbaya zaidi na kuonesha nia ya kutaka kujitoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *