Baada ya Jeshi la Polisi kumtaka katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Vicent Mashinji kuripoti Polisi hatimaye kiongozi ameitika wito huo.
Kiongozi huyo ameitia wito huo wa jeshi la polisi kama ilivyotakiwa na jeshi hilo kufika makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam kufuatia sakata la Tundu Lissu.
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa viongozi ambao wamefika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Chama hicho, Tumaini Makene imesema kuwa katibu mkuu huyo ameitikia wito huo kama alivyotakiwa na jeshi la Polisi nchini.
Taarifa hiyo ilisema kuwa “Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji, akiambatana na wasaidizi wake kutoka Makao Makuu ya Chama, mchana huu, amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Jeshi la Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)”.