Mwanamuziki nyota wa Marekani, Kanye West anatarajia kuzindua siku ya Fashion ijulikanayo kama Yeezy Season 5 Februari 15 mwaka huu jijini New York.
Mkali huyo ameamua kuileta tena Yeezy msimu wa tano baada ya kupata matatizo kwenye Yeezy season 4 ambapo mamodo wake walidondoka kutokana na kuchoka huku wadau wakisema viatu vyake havikua bora.
Kanye West mbali na kuwa mwanamuziki wa Hip Hop pia anajishughulisha na masuala ya mitindo ili kujikusanyia kipato zaidi.
Maonyesho hayo yanatarajia kufanyika Februari 15 mwaka huu katika mji wa New York nchini Marekani.
Mbali na hilo mkali huyo pia anatarajia kuachia nyimbo yake mpya kitendo ambacho mashabiki zake walitazamia kutoka kwa wimbo huo kabla za project nyingine za mwanamuziki.