Nyota wa soka wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu amesema kifo cha mchezaji wa Ivory Coast, Cheick Tiote kinafaa kuwa funzo na kuhakikisha hatua zinachukuliwa kuhusu maradhi ya moyo barani Afrika.

Tiote mwenye miaka 30 alifariki mapema mwezi huu baada ya kuzirai akifanya mazoezi uwanjani China ambako alikuwa anachezea klabu ya ligi ya daraja la pili ya Beijing Enterprises.

Kanu ambaye pia alikabiliana na matatizo ya moyo wakati wa uchezaji wake anasema wakati umefika kwa hatua kuchukuliwa kuhusu maradhi ya moyo uwanjani nan je ya uwanja.

Mchezaji huyo wa Nigeria aliacha kucheza kwa miezi tisa baada ya madaktari kugundua kasoro kwenye moyo wake Inter Milan.

Ilikuwa ni miezi kadha baada yake kusaidia taifa lake kushinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki 1996 mjini Atlanta.

Hata hivyo, aliweza kurejelea uchezaji wake baada ya kufanyiwa upasuaji Ohio, Marekani.

Tiote amejiunga na orodha ndefu ya wachezaji wa Afrika ambao wamefariki uwanjani kutokana na maradhi ya moyo.

Mchezaji huyu wa zamani wa Ajax Amsterdam, Inter Milan, Arsenal na Portsmouth FC anasema atachangia kukabili tatizo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *